24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mihayo awahasa wanaoboresha daftari la wapiga kura

Na YOHANA PAUL -MWANZA

KAMISHINA wa Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC), Jaji mstaafu Thomas Mihayo, amewataka watumishi wote waliopewa dhamana ya kusimamia uandikishaji na uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura, kutekeleza jambo hilo kwa umakini na kwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona.

Jaji Mihayo aliyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akifungua semina kwa mawakala waliopewa dhamana ya kusimamaia zoezi hilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa ambapo alisema kuanza kwa mchakato huo ni hatua za awali za kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba.

Alisema uboreshaji wa taarifa za wapiga kura, utahusisha pia wasimamizi wa ndani na nje ya nchi hivyo dosari za aina yeyote zinaweza kulichafua taifa kuelekea uchaguzi mkuu na kuleta taswira ya tofauti.

 “Tunapoenda kutekeleza jukumu hili tutambue kuwa suala la uboreshaji wa taarifa za wapiga kura ni la kikatiba na kidemokrasia na kwa kuwa nchi yetu inaongozwa kwa misingi hiyo, iwapo tutakamilisha mchakato huu kwa ufasaha itatupatia muongozo mzuri kuelekea uchaguzi mwaka huu.

“Aidha nitumie nafasi hii kuwakumbusha wasimamizi wote mlioteuliwa kukamilisha zoezi hili, kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona kama inavyoelekezwa na Wizara ya Afya nasi kama NEC tumejipanga kutoa vifaa vyote vya kujikinga na tutatoa maelekezo kwa Watanzania jinsi gani wataweza kukamilisha zoezi hili kwa njia ya simu ili kuepusha misongamano,” alisema Jaji Mihayo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Thomas Rutachunzibwa, alisema wakati wa uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kila mmoja achukue tahadhari dhidi ya corona pasipo kujali nafasi yake kwani ugonjwa huo hadi sasa hauna tiba.

Pia aliwasisitiza wateule wa kusimamia zoezi la uboreshaji taarifa za wapiga kura wasitumie vibaya tahadhari ya corona kwani wapo wananchi watajihisi kama wananyanyapaliwa badala yake watoe maelekezo ya njia sahihi zitakazosaidia kujikinga kueneza virusi hivyo wakati wa utekelezaji zoezi hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba aliwataka wasimamizi wa uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kuvitunza vifaa watakavyotumia kwani vifaa hivyo vimenunuliwa na serikali kwa gharama kubwa sana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles