27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Kipenka astaafu utumishi wa umma

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

ALIYEKUWA Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Kipenka Mussa amestaafu kazi ya utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.  

Akizungumza na gazeti juzi, Jaji  Mussa alisema kwa mujibu wa Ibara  ya  120(1) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatamka Jaji wa Mahakama ya Rufani kustaafu kazi hiyo akiwa na umri wa miaka 65.

” Disemba 28, ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwangu,pia siku hiyo  nilistaafu kazi rasmi….namshukuru Mungu nimestaafu kazi hii ya utumishi wa umma niliyoitumikia kwa muda mrefu salama”.

Mussa kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Rais Jakaya Kikwete alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda mbalimbali ikiwemo  Arusha,  Tanga, Bukoba.

Jaji Mussa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa Mahenge . Tume hiyo iliundwa na Rais Kikwete ambayo ilipewa jina la “Tume  ya Jaji Kipenka’  ilimhoji aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam ( ACP- Abdallah Zombe na maofisa wengine wa polisi kwa tuhuma za mauaji ya wafanyabiashara hao.

Jaji Mussa aliwahi kuwa Katibu wa Bunge, wakili wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Haki za Binadamu  ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles