23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Chande: Migongano ya maslahi ni ishara ya hali ya hatari

Na SARAH MOSES, DODOMA.

JAJI Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande, amesema migongano ya maslahi ni ishara ya hatari, hivyo lazima idhibitiwe, na ibainishwe kwani inaweza kuipa sifa mbaya Serikali na watendaji.

Hayo aliyasema jana jijini Dodoma wakati akizindua mjadala wa maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa ambapo alisema mapambano ya migongano ya maslahi ipo na inaendelea ulimwenguni kote.

Alisema kuwa uelewa, utambuzi na uchambuzi makini wa mgogano wa maslahi kwa viongozi na watumishi lazima uzingatiwe kwani moja ya chimbuko lake muhimu ni maadili,pili utumishi wa umma kama jukumu.

Alisema kuwa changamoto kwenye maadili,haki za binadamu,vita dhidi ya rushwa ni kutambua kutawala na kudhibiti mapema migongano ya maslahi kwa njia ambayo italingana kulinda maamuzi ya vitendo kutokana na kushawishiwa visivyo.

“Wakati mwingine viongozi wa umma lazima mkubali kujivua nyazifa mlizonazo ili kulinda heshima yenu ,lazima tukubali kuwa kuna maisha baada ya uongozi ,” alisema Chande.

Vilevile alisema baadhi ya viongozi wa umma wamekuwa wakishindwa kuwa na maamuzi mazuri katika kutekeleza majukumu yao kwa manufaa binafsi hali inayokiuka maadili na hali za binadamu.

“Jambo hili lazima tulitilie mkazo ,lazima tuziishi haki za kibinadamu wakati wa uwajibikaji wetu ili tuepuke mgongano wa maslahi na matumizi mabaya ya madaraka,” alisema.

Kwa upande wake mtoa mada katika mdahalo huo kutoka Chuo Kikuu cha Biashara Dodoma (CBE)Mhadhiri Godfrey Ngh’umbi alisema kuwa mgongano wa maslahi katika utumishi wa umma unapaswa kufanyiwa tathmini kwa mapana ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo sugu la rushwa.

“Rushwa imekuwa ni kikwazo cha kukwamisha maendeleo miongoni mwa taasisi za umma na kusababisha matumizi mabaya ya madaraka”alisema Ngh’umbi.

Naye James Jesse ,Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam alieleza kuwa ,kashfa nyingi zinazowakumba baadhi ya viongozi wa umma zinasababishwa na  mgongano wa maslahi .

Pamoja na hayo alisema kuwa ili kuepuka suala hilo La mgongano wa maslahi lazima kufuata kanuni za utawala bora katika maeneo yote na kuwa na makubaliano ya moja kwa moja katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.

“Haki lazima iendane na kutimiza wajibu,kila mtu kwa nafasi yake akitimiza wajibu wake tutakuwa tunapunguza mgongano wa maslahi katika utumishi wa umma na kuchochea maendeleo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles