NYOTA wa muziki nchini Kenya, Charles Kanyi ‘Jaguar’, ameonyesha jeuri ya fedha kwa kumnunulia mwalimu wake wa zamani, Evanson Gathigu, gari aina ya Toyota Rav4.
Jaguar alitoa zawadi hiyo kwa kudai kwamba maisha yake yamebadilika kutokana na elimu aliyoitoa kwake kwa kuwa yeye ndiye aliyemfanyia mpango wa shule.
“Gathigu alikuwa mwalimu wangu mkuu na yeye ndiye alinifanyia mpango katika shule yake baada ya kukata tamaa ya masomo kutokana na kifo cha mama yangu.
“Nitaendelea kumshukuru mwalimu huyo kwa kuwa bila yeye nisingeweza kufika hapa, ameweza kuyabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa,” alieleza Jaguar.