27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jafo: Msongo wa mawazo unatesa madereva wa Serikali

Christina Gauluhanga Na Chelsea Tillya (UDSM

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali  za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amesema wamebaini chanzo cha madereva wa Serikali kupata ajali mara  nyingi.

Alisema chanzo kikubwa ni msongo wa mawazo ambao hutokana na mabosi wao kukaa na fedha za mafuta na matengenezo ya magari.

Jafo alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana, wakati akikabibidhi magari 30 kwa maofisa elimu wa mikoa inayofuatilia utekelezaji wa elimu.

Alisema hakuna kitu ambacho huenda kinawakera madereva wa magari ya umma kama fedha za ukarabati kahifadhiwa na mabosi.

“Tabia ya fedha za ukarabati wa gari na mafuta kukaa kwa  bosi,  inawakera madereva.

“Sasa naomba fedha hizo zibaki kwa madereva ili kurahisisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati tofauti na ilivyo sasa, ambapo madereva wengi wamekuwa na msongo wa mawazo unaosababisha ajali nyingi hapa nchini,” alisema Jafo.

Akikabidhi magari hayo, Jafo aliagiza maofisa hao kuhakikisha yanafanya kazi ikliyokusudiwa ambayo ni kufuatilia utekelezaji wa elimu tu.

Alisema shule za sekondari za Serikali zitaboreshwa kwa kujengewa mabweni, kuongezwa madarasa, vyoo na nyingine kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha sita.

Alisema wamedhamiria kufanya hivyo kwa sababu katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, shule hizo zimeonekana zikifanya vizuri kwani takribani 52 zimeingia katika 100 bora kitaifa.

“Nawahimiza maofisa hawa kuhakikisha wanasimamia vizuri programu ya elimu bila malipo kwa kuwa wakali ili kuwasaidia wananchi masikini na lengo kuu ni kutokomeza ujinga ndani ya jamii,” alisema Jafo.

Alisema changamoto iliyokuwepo ni maofisa wa elimu kutokuwa na magari na kushindwa baadhi yao kufanya kazi kwa ufanisi.

Kuhusu ukarabati wa shule, Jafo alisema walianza kukarabati shule kongwe nchini na hadi sasa shule 62 zitafanyiwa kati ya 89 za awamu ya kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles