24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

JAFO ATOA KAULI KALI JANGWANI SEKONDARI

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Seleman Jafo,  amefedheheshwa na matokeo ya Shule ya Sekondari Jangwani na kuagiza hatua za haraka zichukuliwe kurekebisha hali hiyo.

Katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita yaliyotangazwa wiki iliyopita, shule hiyo imekuwa ya 451 kati ya shule 453 nchini.

Akizungumza shuleni hapo leo, Jafo ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufanya marekebisho makubwa shuleni hapo kwa masilahi mapana ya wanafunzi na walimu.

“Shule ya Jangwani ina sifa maalumu na ni tunu kwa nchi yetu, lakini leo imekuwa ya tatu kutoka mwisho, hii ni fedheha ambayo haijawahi kutokea…ninyi mna unyafuzi wa kitaaluma shuleni kwenu,”alisema Jafo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles