24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Jafo akipa mwaka mmoja kiwanda cha China Paper kupunguza matumizi ya kuni

Na Safina Sarwatt Moshi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makumu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ametoa muda wa Mwaka moja kwa Kiwanda cha Karatasi cha China Paper kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kutafuta mbinu mbadala katika uzalishaji wa karatasi na kupunguza matumizi ya makubwa ya kuni ambapo hutumia zaidi ya tani mbili kwa siku.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo juzi mjini moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo amesema kwamba serikali haiwezi kukubaliana na hilo na kutoa mwaka moja kwa kiwanda hicho kutafuta mbadala ikiwemo makaa ya mawe.

“Ninyi mnamikakati gani katika utunzaji wa mazingira, kwani matumzi yenu ya kuni kwa siku ni makubwa mno, hakikishe mnatafuta mbinu mbadala tofauti na kuni, mimi kama waziri wa mazingira nawapa mwaka moja nitarudi tena kuangalia kama maelekezo hayo yametekelezwa,” amesema Jafo.

Amesema kuwa lazima kiwanda kiweke mikakati ya kupanda miti na siyo kusubiri kampeni za serikali za upandaji wa miti.

“Nanyi pia muwe na utaratibu wenu wa kupanda miti na siyo kwamba mnasubiri kampeni za serikali kwani ndiyo mna matumizi makubwa ya kuni,mnapokata miti lazima muwe mnafanya kufidia miti mingine,”amesema Jafo.

Waziri Jafo pia ameitaka kiwanda hicho kutumia taka zinazozalishwa kwandani hapo kama mali ghafi nyingine ikiwemo kutengenezea matofali ya gharama nafuu.

“Mgejiongeza jinsi gani ya kutumia hizo taka kutengenezea matofali ya gharama nafuu badala kuzirudika hapa kutokana na kukosena kwa dampo la kutupa, kwani inajaza dampo haraka wakati kuna uwezekano wa kuanzisha mradi wa matofali au mkaa.

“Angalieni namna ya kushirikiana na manispaa ya Moshi pamoja watalaamu kutoka chuo cha Nelson Madela na kuona ni kwa namna gani mtazitumia hizo taka ili isiathiri mazingira,Mimi kama waziri wa mazingira sitaki kuona uchafu,afuteni njia mbadala,”amesema.

Meneja wa kiwanda cha China Paper, William Mbila amesema kiwanda hicho kwa siku kinatumia zaidi ya tani mbili za kuni katika uzalishaji na kwamba changamoto kubwa upatikaniji wa msitu wao binafsi

Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Lewis Nzali amesema kuwa tayari walishatembelea kiwanda hicho na kuwapa maelekezo na kwamba endapo watashindwa kutekeleza watachukua hatua za kisheria.

Katika ziara hiyo Waziri Jafo pia ametembelea kiwanda cha kutengeneza nondo cha Five Star, dampo la kisasa la Manispaa ya Moshi pamoja Bwawa la maji machafu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles