23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Jafo akerwa na machinjio Tabora

Na Lulu Mussa, Tabora

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Bosco Ndunguru katika kipindi cha siku saba kuhakikisha machinjio katika Manispaa yake yanafanyiwa usafi madhubuti.

Agizo hilo limetolewa leo Mei 12, 2021 na Waziri Jafo marabaada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua usimamizi na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 Mkoani Tabora.

Akiwa katika machinjio hayo Waziri Jafo ameshuhudia kukithiri kwa uchafu ndani na nje ya jengo hilo jambo ambalo linahatarisha afya za wakazi wa Tabora.

“Mazingira ya hapa ni machafu sana, natoa muda wa wiki moja marekebisho yafanyike na nipate taarifa ya utekelezaji mapema iwezekanavyo pia natoa mwezi mmoja wa ukarabati wa mfereji wa maji taka,” amesema Jafo.

Waziri Jafo pia ametembea Kampuni ya kuzalisha mkaa mbadala ya “Kuja na Kushoka” na kutoa rai kwa taasisi za Umma na Binafsi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala unaozalishwa kutokana na taka.

“Azma ya Serikali ni kuhakikisha tunatunza mazingira yetu kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, natoa rai kwa Shule za Binafsi na za Serikali kununua hizi mashine za kuzalisha mkaa badala ili zitumike kuzalisha mkaa katika Shule zao pia kama chanzo cha mapato kwa kutengeza mkaa na kuuzia wengine,” amesema Jafo.

Akiwasilisha taarifa ya Kampuni ya kuzalisha mkaa mbadala, Leonard Kushoka amesema anatumia teknojia ya kuchakata taka na kuzalisha mkaa mbadala ambao umekuwa wa manufaa kwa wakazi wa Tabora na Tanzania kwa ujumla kwa kutoa ajira kwa vijana kunusuru mazingira.

Waziri Jafo yuko mkoani Tabora kukagua shughuli za uhifadhi na usimamizi wa Mazingira ambapo kwa siku ya kwanza amekagua Machinjio ya Manispaa ya Tabora, Kampuni ya kuzalisha Mkaa mbadala na ukaguzi wa mabwawa ya maji taka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles