23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jacob Zuma akana mashitaka 18

Pietermaritzburg, Afrika Kusini

Aliyekuwa Rais wa zamani nchini Afrika Kusini, Jacob Zuma, leo Mei 26, 2021 amesimama kizimbani na kukana mashitaka 18 yanayomkabili dhidi yake.

Katika kesi yake ya msingi iliyosikilizwa Mahakamani jijini Pietermaritzburg, mwanasiasa huyo anakabiliwa na tuhuma za rushwa, ukwepaji kodi na utakatishaji fedha.

Akizungumza kwa upole rais Jacob Zuma mwenye umri wa miaka 79, huku watu wanaomuunga mkono wakiwa wamekusanyika nje ya mahakama, amesema kesi zake ni matokeo ya siasa chafu dhidi yake.

Akifafanua hilo, Zuma hakuwataja majina lakini alisema maadui zake wanatoka ndani na nje ya Chama tawala nchini humo, African National Congress (ANC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles