Ja Rule ataka kumaliza bifu na 50 Cent

0
720

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Jeffrey Atkins, maarufu kwa jina la Ja Rule, ameanza kuonesha dalili za kutaka kumaliza tofauti zake na rapa 50 Cent baada ya kusema haona maana ya kuendelea na mgogoro.

Wawili hao wamekuwa kwenye bifu zito kwa kipindi cha miaka 15 sasa, lakini Ja Rule amesema ni bora ajitoe kwenye mgogoro.

“Tumekuwa kwenye bifu kwa kipindi cha miaka 15 sasa kama sijakosea, lakini kwa upande wangu sioni sababu ya kuendelea kuwa kwenye hali hii, naona ni bora nikajitoa.

“Nimegundua kwamba nikiendelea kuwa kwenye bifu jamii hainielewi, sitaki kuonekana kuwa chanzo, hivyo ni bora nikae pembeni,” alisema msanii huyo.

Lakini kwa upande wa 50 Cent, aliwahi kusema hayupo tayari kumaliza tofauti zao hadi mmoja wao atakapo fariki dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here