MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emanuel Simwiga ‘Izzo Business’, amesema mashabiki wakae tayari kupokea kazi zake.
Akizungumza na gazeti hili jana, Izzo Business, alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi mambo ambayo amepanga katika kipindi hiki cha mwaka huu, ila utakapofika muda ataweka wazi kila kitu ila kwa sasa anajipanga kupambana na ushindani.
“Nataka nizidi kuwaburudisha zaidi mashabiki wangu mwaka huu, kwa kutoa vitu tofauti kabisa hivyo nawaomba wakae tayari kupokea kazi zangu mpya,” alisema Izzo Business.
Msanii huyo amefanikiwa kufanya vizuri kupitia video yake inayokwenda kwa jina la ‘Shemu Lake’ akiwa ameshirikiana na wasanii wenzake kama Mwana FA pamoja na G. Nako.