26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Itumbi afunguka mazito njama za kumuua Rutto

NAIROBI-KENYA

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidijitali katika ikulu ya Kenya, Dennis Itumbi ambaye alikamatwa juzi na polisi kuhusiana na barua ya njama ya kumuua Naibu Rais, William Ruto sasa kubaki rumande kwa siku tano zaidi.

Itumbi ambaye alifikishwa mahakamani jana, waendesha mashataka waliwasilisha ombi la kutaka aendelee kushikiliwa wakati wakichunguza chanzo cha barua hiyo inayodai mawaziri kadhaa walikutana katika hoteli ya Nairobi kupanga jinsi ya kumuua Ruto.

Kabla mahakama ya Nairobi haijatoa uamuzi, Itumbi alimwambia hakimu kuwa ni kweli kulikuwa na mkutano uliofanyika katika hoteli ya La Mada  ambao agenda yake ilikuwa ni kumuua Ruto.

Itumbi alimwambia hakimu kuwa alikuwa na video kuthibitisha madai yake na kuiomba mahakama aionyeshe lakini hakimu hakutoa neno kama aonyeshe video hiyo.

Itumbi alisema alipeleka taarifa hizo hizo kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai  lakini polisi wameonyesha wana nia na yeye kufikishwa mahakamani na si kuangalia ukweli.

Baada ya kusema hayo mahakama iliamuru aendelee kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga ili kuruhusu polisi kuchunguza masuala makubwa aliyoibua.

Wabunge wengi walifika mahakamani jana kwa ajili ya kumuunga mkono Itumbi wakisema wanataka waziri na Katibu Mkuu ambao hawakuwataja kwa majina wachunguzwe juu ya tuhuma hizo za mipango ya mauaji.

‘BARUA FEKI’

Itumbi anashtakiwa kwa kuweka barua hiyo kwenye kundi la WhatsApp la Tangatanga  linalomuunga mkono Ruto.

Alimatwa Jumatano Nairobi wakati akipata chakula cha mchana  na huenda akashtakiwa kwa kuchapisha taarifa za kutishia.

Uchunguzi wa awali kuhusiana na barua hiyo umebaini kuwa tuhuma kwamba mawaziri wanne walikutana kupanga njama za kumuua Ruto, si tu kwamba ni uongo lakini pia barua hiyo iliandikwa na watu wa karibu na Ruto.

Itumbi anafanya kazi katika Ofisi ya Rutto na mahakamani anawakilishwa na wakili Katwa Kigen.

Itumbi alimatwa juzi na wapelelezi wanaochunguza tuhuma za njama za barua za kumuua Ruto.

Juzi kabla ya jana kufikishwa mahakamani gazeti la The Standard la nchini Kenya liliandika kuwa, Itumbi alikamatwa  ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuwapo taarifa za kutambulika kwa chanzo cha barua hiyo iliyozusha tuhuma za kutaka kuuawa Ruto.

Wiki iliyopita, mawaziri waliotajwa kuhusika na mipango hiyo hatari walikana kupanga njama za kumuua Ruto.

Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa Waziri wa biashara wa Kenya, Peter Munya alikana shutuma za kupanga mauaji ya Ruto.

Waziri Munya alikuwa akizungumza nje ya makao makuu ya ofisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambako aliitwa sambamba na mawaziri wengine, kuhojiwa kuhusu shutuma kuwa walimtishia Ruto.

Gazeti la The Standard liliripoti kuwa mawaziri hao walishutumiwa kufanya vikao vya siri, lakini Munya aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawajapeleka taarifa polisi kwa kuwa Ruto hajapeleka malalamiko rasmi.

Gazeti la Daily Nation la Kenya lilimnukuu waziri  huyo akisema kuwa Ruto alidai kuwa mawaziri hao walikuwa wakifanya vikao vya siri na maafisa wengine.

Sakata hili la sasa limekuja wakati Ruto mwenye akiwa na mipango ya kuwania urais mwaka 2022.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles