24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

ITC YAMCHELEWESHA BEKI MPYA YANGA

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KUCHELEWA kwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC), imepelekea kumchelewesha mchezaji mpya wa Yanga, Fiston Kayembe, kuanza kucheza kwenye kikosi hicho.

Fiston alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) klabu ya Balende FC katika dirisha dogo la usajili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa klabu huyo, Boniface Mkwasa, alisema kwa sasa wanaendelea kufuatilia hati hiyo na muda wowote kuanzia sasa itakuwa imepatikana.

“Kayembe hakuweza kucheza kutokana na ITC yake kuchelewa, lakini kwa sasa tunaendelea kuifuatilia na itakapokuwa tayari basi ataanza kucheza,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mkwasa alisema wamefikia hatua nzuri katika kujaza kifusi kwenye uwanja wao ambapo wanatarajia ifikapo msimu ujao utakuwa tayari kwa matumizi.

Alisema wanatoa muda wa miezi miwili endapo hawatafanya hivyo, basi watalifikisha suala hilo katika sehemu husika ya mazingira.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Dismas Ten, alisema hadi sasa wameshatuma majina 20 CAF ya wachezaji huku mengine saba wakitarajia kutuma muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Tunafahamu mwisho wa kutuma majina hayo CAF ni Desemba 31, mwaka huu na sisi tumeshatuma 20, lakini mengine saba tulichelewa kwa sababu mtandao ulikuwa unasumbua hivyo ndani ya saa 24 yatakuwa tayari tumetuma.”

Yanga ambayo inashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika, imepangwa kuanza na timu ya St. Louis ya visiwani Shelisheli huku Simba ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho ikipangwa kucheza na Gendarmerie Nationale ya Djibouti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles