24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

ITALIA YATUMBUKIA KATIKA MZOZO MPYA WA KISIASA

ROME, ITALIA


ITALIA imetumbukia katika mgogoro mpya wa kisiasa baada ya jitihada za vyama maarufu kutaka kutwaa madaraka kusambaratika, huku rais akitarajiwa kumteua mchumi atakayeiongoza Serikali ya wasomi kabla uchaguzi mpya kufanyika.

Rais Sergio Mattarella alitumia kura yake ya turufu kuzuia uteuzi wa Paolo Savona kama Waziri wa Uchumi, hatua iliyowakasirisha viongozi wa vuguvugu la nyota tano na Chama cha League na kumfanya Waziri Mkuu wao mteule, Guiseppe Conte kujiondoa.

Mattarela amesema alikubali uteuzi wa mawaziri wote isipokuwa Savona, ambaye ameiita sarafu ya euro kama ‘kifungo cha Ujerumani’ na kusema Italia inahitaji mpango wa kuondoka kutoka ukanda unaotumia sarafu ya euro.

Viongozi wa vuguvugu la nyota tano na Chama cha League wamelaani vikali kura hiyo ya turufu ya rais kwa kile walichokiita kuwa ni hatua ya Ujerumani, mashirika na makundi ya ushawishi wa kifedha kuingilia siasa za Italia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles