Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Chuo Cha Kodi (ITA) nchini kimetakiwa kufanya utafiti wa kutatua changamoto za forodha na kodi ili kupata suluhu ya ukwepaji kodi na kubuni vyanzo vipya vya ulipaji.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande leo Novemba 24,2023 kwenye mahafali ya 16 ya Chuo cha Kodi, jijini Dar es Salaam.
Chande serikali inawategemea wahitimu hao kutatua changamoto mbalimbali na kuboresha mfumo wa kodi na forodha.
“Katika utafiti utakaofanywa uende kutatua changamoto za forodha nakodi na kuleta suluhu ili watu walipe kodi kwa hiyari na kodi stahiki iwe inakusanywa kwa wakati, “amesema.
Amesema Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) inawajibu wa kusaidia kupanua wigo kwa wadau wengi ili serikali ipate wataalamu wa katika eneo hilo.
Chande amesema walipa kodi wengi elimu yao ni ndogo, wamebaini changamoto hiyo, hivyo Chuo cha Kodi kianzishe kozi fupi kwa ajili ya walipakodi
” Washauri wengi wa walipakodi wana taaluma ya upande mmoja, inabidi wawe na taaluma ya kodi na uhasibu ili waweze kuwa washauri wazuri katika masuala ya kodi,”amesema.
Aidha amewataka wahitimu kutokana na taaluma zao, wakaanzishe kampuni na kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho kwa kufanya kazi kwa waledi.
Amewaomba wahitimu hao kuwa wanakwenda mtaani na huko kuna mambo mengi wakafanye mambo ambayo yanaendana na maadili ya kitanzania.
Naye Kamishina Mkuu wa TRA , Alphayo Kidata, amesema wakaendeleze elimu waliyopata kuleta maendeleo kwa jamii.
“Yale mliyosomea na mambo ya kodi mkafanye kazi kwa waledi na mkalete maendeleo ya Taifa na kukuza uchumi kupitia elimu zenu,”amesema Kidata.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Isaya Jairo, amesema chuo ni mhimili wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) katika kukidhi mahitaji ya mafunzo kwa watumishi wake kwa asilimia 70.
“Kila mwaka wafanyakazi wa mamlaka hiyo wanapata mafunzo katika chuo cha kodi, katika mwaka wa masomo wa 2022/23 jumla ya wahitimu 508 wamefuzu masomo yao na wanatarajia kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali, “amesema Profesa Jairo.