32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

ITA YAJIVUNIA KUWANOA WAFANYAKAZI

Meneja Mafunzo na Maendeleo ya Watumishi wa TRA, Yasin Mwita

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

CHUO cha Usimamizi wa Kodi Tanzania (ITA), kimesaidia kukuza uelewa kwa watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwaongezea ufanisi katika ukusanyaji kodi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho miaka kumi iliyopita.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mafunzo na Maendeleo ya Watumishi wa TRA, Yasin Mwita, katika onyesho la vipaji na uwezo lililoandaliwa na Serikali ya wanafunzi na uongozi wa chuo hicho.

Alisema ameshuhudia uwezo mkubwa uliooneshwa na wanafunzi hao katika kufanya mambo mbalimbali waliyojifunza ikiwa ni pamoja na namna ya kutoa huduma kwa weledi na kuzingatia sheria.

“Tumeona jinsi gani wanaweza kuwasilisha na kuonesha kwa vitendo walichojifunza, huu ni msaada mkubwa kwetu TRA na wadau wetu wengine, nasi tunatoa zawadi kwao kama motisha ya kuwafanya hata wafanyakazi kuona haja ya kujiendeleza,” alisema Mwita.

Aliongeza kuwa TRA itaendelea kukiunga mkono chuo hicho kuanzisha na kuwezesha mafunzo mbalimbali kuhakikisha kinafika malengo waliyojiwekea.

“Ni matumaini yangu kuwa yale yaliyooneshwa hapa yataleta matokeo chanya kwa wanafunzi na wanataaluma nzima ya wakusanya kodi,” alisema Mwita.

Naye Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma, Lewis Ishemoi, alisema katika kipindi chote cha miaka kumi ya chuo hicho kimekuwa kikifanya jitihada kubwa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TRA na taasisi nyingine.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,579FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles