POLISI wa Israel wanaendelea kuwashikilia raia wa Palestina 2,800 tangu Mei, mwaka huu, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Safa.
Wapalestina hao ni wale waliokamatwa baada ya maandamano yaliyoua watu zaidi ya 250 katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa mwanasheria Khaled Zabarqeh, Wapalestina 40 wamefunguliwa mashitaka ya kuwaua Waisrael, huku 35 wakiendelea kusota magerezani.
Aidha, mwanasheria huyo anaamini hao 40 waliofikishwa kwenye mahakama wa Israel watakumbana na hukumu nzito.