27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Israel yashambulia Islamic State

Israel

JESHI la Israeli, linasema limefanya mashambulio ya anga dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina mjini Gaza na Syria kujibu mashambulio yake ya roketi.

Jeshi hilo, linasema limeyapiga maeneo ya jihad kusini mwa mji mkuu wa Syria, Damascus na  ukanda wa Gaza siku ya Jumapili.

Katika hatua ya nadra ya Israeli kukubali mashambulio dhidi ya Syria, jeshi la lilisema lililenga ” kitovu cha shughuli za kundi la jihadi la Kiislamu”

Syria imesema  majeshi yake ya ulinzi ya anga yalidungua makombora mengi ya Israeli.

Watu wanee walijeruhiwa mjini Gaza, kulingana na maofisa wa afya, lakini hakuna ripoti za moja kwa moja juu ya vifo kutokana na mashambulio ya Israeli.

Mashambulio yalifanywa baada ya eneo la kusini mwa Israeli kupigwa na kundi la makombora takriban 20 ya roketi yaliyorushwa mapema Jumapili. Hakuna ripoti juu ya majeruhi kwa upande wa Israeli

Uhasama huu ulianza Jumapili, wakati Israeli iliposema ilimuua mjumbe wa kikundi cha Jihad maeneo ya uzio wa mpaka na ukanda wa Gaza.

Taarifa zinasema mwanaume huyo alikuwa akijaribu kuweka mtambo wa vilipuzi.

Ukanda wa video uliosambazwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii, ilionyesha tingatinga la Israeli likiuburuza mwili wa mtu huyo, jambo lililoibua ghadhabu miongoni mwa Wapalestina.

Baadhi ya Wapalestina walitoa wito wa ulipizaji kisasi na saa kadhaa baadae, maroketi yakafyatuliwa  ukanda wa Gaza na ndipo uvamizi wa anga ukaanza.

Kundi la Jihad la Kiislamu lilidai kuhusika na shambulio la maroketi, likiyataja kuwa ni jibu la mauaji ya mmoja wa wapiganaji wake aliyeuliwa kwenye eneo la mpaka wa Gaza.

Kundi hilo linaungwa mkono na Iran, ni mojawapo ya makundi yaliyo imara zaidi ya wanamgambo katika Gaza. Likiwa ni mshirika mkuu wa Hamas, limekuwa likipigana vita kadhaa dhidiya Israeli katika miongo ya hivi karibuni.

Unaweza pia kusoma:

Mapigano baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Jihad yalishamiri Novemba,mwaka jana, wakati mashambulio ya anga ya Israeli yalipomuua kamanda wa ngazi yajuu wa kikundi cha wanamgambo mjini Gaza.

Makabiliano baina ya vikosi vya Israeli na Wapalestina yalishuhudiwa mapema mwezi huu pia, siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donal Trump kutangaza mpango wake wa amani na kufungua ubalozi wa Marekani mjini Jerusalemu.

Rais trump alisema kuwa “Hakuna Wapalestina wala Waisraeli watakaotolewa katika makazi yao”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles