30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

IRELAND YARUHUSU KUTOA MIMBA

DUBLIN, IRELAND


IRELAND imepitisha kwa asilimia kubwa kura ya maoni ambayo inaondoa sheria kali za kutoa mimba katika Taifa hilo la Kikatoliki.

Waziri Mkuu Leo Varadkar, ambaye aliunga mkono kura hiyo ya maoni, amesema ni tukio la kihistoria hatimaye kufuta miongo mingi ya unyanyapaa na aibu.

Zaidi ya asilimia 66 ya wapiga kura katika nchi hiyo, waliunga mkono kura hiyo inayoondoa marufuku ya kikatiba ya utoaji mimba huku asilimia 33.6 ikipinga.

Juzi maelfu ya watu waliojawa furaha kufuatia kupitishwa kwa kura hiyo ya maoni walishangilia mjini Dublin.

Kwenye hotuba yake, Waziri Mkuu Varadkar alisema anataka sheria hiyo mpya ianze kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu.

Matokeo hayo ni pigo jingine kwa Kanisa la Katoliki nchini hapa kwa vile limejiri miaka mitatu tu baada ya kura nyingine ya maoni kuhalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles