25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Iran yatoa msimamo makubaliano ya nyuklia

TEHRAN- IRAN

IRAN imetoa msimamo wake mpya ikisema itapunguza zaidi kuzingatia majukumu yake chini ya makubaliano ya kinyuklia na mataifa yenye ushawishi mkubwa zaidi duniani na kuongeza kiwango cha urutubishaji wa madini ya Urani kuliko kile kilichokubaliwa cha kutengeneza mafuta ya vinu vya nyuklia.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia wanasema msimamo huo mkali wa Iran unaashiria kuchukizwa zaidi na matokeo ya changamoto inazokabiliana nazo za ongezeko la shinikizo la vikwazo kutoka Marekani.

Katika mkutano na Waandishi wa habari, maofisa wakuu wa serikali ya Iran wamesema kuwa Iran itaendelea kupunguza uzingatiaji wake wa mkataba huo baada ya kila siku 60 iwapo mataifa yaliotia saini mkataba huo hayatachukua hatua za kuilinda dhidi ya vikwazo vya Marekani.

Pamoja na msimamo wake huo imeaacha mlango wazi kwa ajili ya  ufumbuzi wa kidiplomasia.

Katika dalili ya kuongezeka kwa wasiwasi kutoka kwa mataifa ya Magharibi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema yeye na Rais wa Iran, Hassan Rouhani wamekubaliana kutafuta namna ya kuanzisha tena mazungumzo kuhusiana na suala hilo kufikia Julai 15, mwaka huu.

Pamoja na hayo Macron amemuonya Rouhani, kwamba ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kudhoofishwa zaidi mkataba wa nyuklia wa Iran uliofikiwa mwaka 2015 na kuonya kuwa madhara yatafuata

Macron aliyasema hayo alipozungumza na Rouhani, siku moja kabla ya Iran kujiandaa kuongeza urutubishaji wa madini ya urani kupita kiwango kilichowekwa katika makubalino yake na mataifa makubwa.

Amesema anataka kuweka msukumo wa kufanyika mazungumzo kuanzia sasa na Julai 15, kwa lengo la kuzirudisha pande zote katika meza za mazungumzo.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Ufaransa Macron ilieleza; ” Rais ameonesha wasiwasi mkubwa, kutokana na hatari viashiria vya udhoofishiji wa mkataba wa nyukilia wa mwaka 2015, na madhara ambayo yatakufuata,”

 Hata hivyo taarifa hiyo haikuwekwa wazi madhara ambayo inayazungumzia.

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema kuendelea kukiukwa zaidi kwa mkataba huo, kunaweza kusababisha mtibuano wa muundo wa maazimio ndani ya mkataba wenyewe upande wa Ulaya yaani Ufaransa, Uingereza na Ujerumani.

Jambo ambalo wanasema linaweza kuchangia kuzushwa kwa uwekwaji wa vikazo vya Umoja wa Mataifa.

Iran imetoa takwa la kuyataka mataifa ya Ulaya kufanya jitihada zaidi, katika kuhakikisha inapata manufaa ya kiuchumi, na hasa katika sekta yake ya mafuta ambayo Marekani imekuwa ikiilenga.

Macron amesema pamoja na Iran kutoa tarehe ya mwisho ya Julai 7, lakini amekubaliana na Rouhani kufanyika jitihada kuanzia sasa hadi Julai 15, kurejesha mazungumzo kwa pande zote.

Hata hivyo kwa upande wa Iran, haujaonekana kuunga mkono mazungumzo hayo kama vikwazo vyote ilivyowekewa havijaondolewa.

Katika  televisheni ya umma ya Iran, Rais Rouhani amesikika akisema kuondolewa kwa vikwazo kwa taifa lake kutatoa fursa wa mwelekeo mpya.

DW

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles