24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Iran yatangaza uamuzi mzito kuhusu mpango wake wa nyuklia

TEL-AVIV-IRAN

MSEMAJI wa Shirika la Nguvu za Atomiki nchini Iran, Behrouz Kamalvandi amesema nchi hiyo itaondoa ukomo wa kiwango cha ulimbikizaji madini yake yanayotumika kutengeneza silaha hatari za nyuklia (uranium)  kilichoafikiwa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia.

Alisema uamuzi huo utafanyika, katika kipindi cha siku 10 zijazo. 

Kamalvandi ametowa kauli hiyo katika mkutano na waandishi habari ulionyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni ya Taifa ya Iran jana. 

Kauli hiyo ya Iran imekuja katika wakati ambao hisia za kuishuku nchi hiyo kwamba ilihusika na mashambulizi dhidi ya meli za mafuta wiki iliyopita katika eneo hilo, zikiwa zimetanda.

Serikali ya Marekani imeilaumu Iran wakati pia kukiweko hali ya kuongezeka hali ya wasi wasi kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa msemaji huyo wa shirika la nguvu za atomiki wa Iran, tayari nchi hiyo imeongeza mara tatu kiwango cha uzalishaji wa madini ya Urani ya viwango vya chini.

Wakati huo huo, Ripoti mpya iliyochapishwa jana imeonyesha kiwango cha silaha za nyuklia duniani kimepungua katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita lakini mataifa ulimwenguni yanatengeneza silaha za kisasa zaidi.

Kulingana na makadirio ya Kituo cha kimataifa cha utafiti wa amani cha Stockholm (SIPRI) mwanzoni mwa mwaka 2019 mataifa tisa ulimweguni yalikuwa na shehena ya silaha 13,865 za nyuklia. 

Idadi hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na mataifa ya Marekani, Urusi, uingereza, ufaransa, China, india, Pakistan, Israel na Korea kaskazini ni pungufu ya silaha 800 za nyuklia ikilinganishwa na mwaka 2018. 

SIPRI imesema mataifa yenye silaha za nyuklia yanaboresha shehena zao za silaha huku China, India na Pakistan zinaongeza kiwango cha silaha zake za nyuklia.

SIPRI imesema mafanikio hayo yanatokana na mataifa ya Urusi na Marekani kutimiza wajibu wake kwenye mkataba wa mwaka 2010 unaoweka kikomo cha umiliki wa silaha za nyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles