21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Iran yakiri kudungua ndege ya Ukraine kimakosa

TEHRAN, IRANĀ 

JESHI la Iran hatimaye limekiri kudungua kimakosa ndege ya abiria Ukraine Jumatano wiki hii, runinga ya taifa ya Iran imeripoti.

Taarifa ya jeshi inaeleza kuwa mkasa huo umetokana na makosa ya kibinadamu baada ndege hiyo kupita karibu na eneo nyeti linalomilikiwa na Kikosi cha Mapinduzi (Revolutionary Guards).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Maofisa waliofanya kosa hilo wataadhibiwa

Iran awali ilikanusha vikali taarifa kuwa moja ya makombora yake  iliyokuwa ikiyarusha kuelekea ziliko kambi za kijeshi za Marekani nchin Iraq yaliitungua ndege hiyo karibu na mji mkuu Tehran.

Watu wote 176 ndani ya ndege hiyo wamepoteza maisha.

Hata hivyo nchi hiyo ilikabwa koo baada ya Marekani na Canada kudai kuwa taarifa za kijasusi walizonazo zinaonesha kuwa Iran iliidondosha ndege hiyo kwa bahati mbaya na moja ya makombora yake.

Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Vyombo vya habari vya Marekani vinadai kuwa Iran ilidhani kuwa ndege hiyo ilikuwa ya kivita ya Marekani, wakati taifa hilo lilipokuwa ikijiandaa kujibu mashambulio dhidi ya Marekani baada ya wao kushambulia vituo vyake vya kijeshi nchini Iraq kwa makombora.

Iran ilirusha makombora kwenye kambi za Marekani Jumatano kama sehemu ya kisasi chake baada ya rais Donald Trump wa Marekani kuagiza shambulio la anga lililomuua Jenerali wa Iran Qasem Soleimani Januari 3.

Kanda ya video iliyopatikana na gazeti maarufu la Marekani la New York Times ilionesha jinsi makombora yalivyokuwa yakipita katika anga la Tehran na baadae kulipuka ilipokutana na ndege hiyo.

Karibu sekunde 10 baadae mlipuko mkubwa ulisikika ardhin.

Rais Trump siku ya Alhamisi alisema nina shaka juu ya (kuanguka) kwa ndege. “Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa.”

VIKWAZO VIPYA DHIDI YA IRAN

Wakati huo huo, Marekani imetangaza vikwazo vipya vya kiuchumi kwa Iran kutokana na hatua yake hiyo ya kurusha makombora kufuatia mashambuli kwenye kambi za jeshi la Marekani nchini Iraq. 

Waziri wa Mambo ya Nje  wa Marekani, Mike Pompeo na Waziri wa Fedha, Steven Mnuchin wamesema vikwazo vipya vitawalenga maofisa wanane wa ngazi ya juu wa Iran. 

Maofisa hao ni wale wanaohusika na kile Marekani ilichokitaja kuwa ni shughuli za kudhoofisha usalama wa mashariki ya kati pamoja na mashambulizi ya makombora ya siku ya Jumanne. 

Vikwazo vitawekwa pia kwa wote wanaohusika na sekta ya nguo, ujenzi, madini, chuma na uzalishaji viwandani nchini Iran kwa lengo la kupunguza mapato ya kifedha kwa Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles