TEHRAN, IRAN
Serikali ya Iran imewekea shinikizo Ujerumani kuonyesha matokeo ili kuokoa mkataba wa nyuklia ikisema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas lazima achukue hatua wakati wa ziara yake nchini humo leo Jumatatu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif alinukuliwa na kituo cha habari cha kitaifa nchini humo akisema kuwa kuhusiana na mkataba huo wa kinyuklia, matokeo ndio yanayojalisha na kuongeza kuwa anataka kujuwa kilichoafikiwa na washirika ili kuuokoa.
Mwaka jana , Marekani ilijiondoa katika mkataba na Iran ambao ulilenga kuizuia nchi hiyo kutengeza silaha za nyuklia na imeanza kutekeleza vikwazo dhidi ya sekta za mafuta na benki ambavyo vimeuporomosha uchumi wa Iran.