IRAN NA KAMPUNI YA TOTAL KUSAINI MKATABA WA GESI LEO

0
848

Iran inatarajia kusaini mkataba baina yao na kampuni kubwa ya uchimbaji mafuta na gesi Total ya Ufaransa wa karibu dola bilioni tano.

Kwa mujibu wa mtakaba huo wenye thamani ya dolla billioi 5 , kampuni ya Total itaendeleza uchimbaji na uhifadhi wa gesi katika maeneo ya kusini mwa bahari ya Iran, liitwalo Pars gas ikiwa ni mojawapo ya mikataba mikubwa zaidi ya kibiashara kuwahi kufanywa na Iran tangu iondolewe vikwazo vya kiuchumi.

Mafisa wa wizara ya mafuta walisema kuwa mkataba huo ni wa kujengwa kiwanda cha gesi ambapo Total itapa asilimia 50.1.

Maafisa katika Wizara husika wanasema makubaliano hayo yatawekwa saini leo huko mjini Tehran.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here