22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

‘Ipo siku nitaiwakilisha Tanzania Kimataifa’

Finlay akiwa amerudisha mpira kwa mwalimu wake (hayupo pichani)
Finlay akiwa amerudisha mpira kwa mwalimu wake (hayupo pichani)

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

KILA mwanadamu hapa duniani anatamani siku moja familia na Taifa lake limkumbuke kwa kufanya kazi kwa bidii ambayo itaacha alama ya ukumbusho baada ya maisha yake ya hapa duniani.

Matumaini hayo yapo pia kwa Finlay Shayo mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Academic iliyoko Mikocheni, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Natamani siku moja niweze kuiwakilisha nchi yangu katika mashindano makubwa ya Kimataifa na kurejea na ushindi nyumbani, naamini hiyo itanipa heshima kubwa mimi binafsi, familia na Taifa langu kwa ujumla,” ndivyo aanavyosema Shayo katika mahojiano na gazeti hili.

Anasema ili kufikia jambo hilo atahakikisha anajitahidi kufuata maelekezo yote anayopewa na mwalimu wake wa tenisi mchezo ambao anaupenda kwa dhati.

“Naomba Mungu usiku na mchana ili anisaidie siku moja jabo hili liweze kulitimiza, navutiwa mno na mchezo huu na naamini kuwa ipo siku nitafanikiwa,” anasema.

Anasema kila anapokaa kutazama luninga na kuona mataifa mengine yakishinda katika kila shindano huku Tanzania ikiwa inashindwa mara nyingi amekuwa akihuzunika sana.

“Huwa nashindwa kula, najisikia uchungu nchi yetu ikikosa ushindi, naamini wapo wachezaji wazuri katika timu ya Taifa lakini nafikri serikali inapaswa kuwekeza zaidi,” anasema.

Anasema uwekezaji unaopaswa kufanywa ni pamoja na kusaka vipaji vya watoto kama yeye na kuwapatia mafunzo zaidi.

“Binafsi naupenda mchezo huu na nashukuru familia yangu ilikubali kunitafutia mwalimu hapa katika klabu ya tenisi ya Kijitonyama ambako napata mafunzo.

“Lakini bado kuna vipaji vipo huko katika shule nyingine, si wazazi wote wanaweza kuleta watoto wao kuja kujifunza hapa hivyo ni vyema mchezo huu nao ukafundishwa shuleni kama ilivyo kwa mpira wa miguu,” anasema.

Anasema iwapo serikali itawekeza katika mchezo wa tenisi itasaidia kupata vipaji vingi na kutengeneza timu bora ya Taifa na fursa kubwa ya Tanzania kuibuka na ushindi katika michuano mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa pia.

“Lakini wapo wazazi wengine ambao naweza kusema wamekuwa wakichochea kuua vipaji vya watoto wao, anaona mtoto wake ana uwezo wa kucheza mchezo fulani lakini anamzuia lile si jambo jema kwa sababu linaua kipaji cha mtoto husika,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles