27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

INI, FIGO NA MOYO WA MAREHEMU KUTUMIWA NA WATU WENGINE

Na ESTHER MNYIKA-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), inatarajia kupeleka mapendekezo serikalini uandaliwe muswada wa sheria kuruhusu kuchukuliwa moyo, figo na ini kutoka kwa marehemu, vitumiwe na watu wengine.

Mkurugenzi wa Upusuaji wa taasisi hiyo, Dk. Bashir Nyangasa, alisema Dar es Salaam jana kuwa JKCI inao uwezo wa kupandikiza viungo hivyo vya mwili kwa binadamu.

“Umefika wakati kwa Watanzania kujiwekea utaratibu wa kuacha wosia wa kutumika kwa viungo vyao baada ya kufariki dunia, vihifadhiwe katika benki za viungo viweze kutumiwa na watu wengine wenye uhitaji.

“Utaratibu huo kwa nchi za wenzetu upo na sheria zipo na mtu ana uwezo wa kusema ‘kama nikifa maini, figo na moyo vichukuliwe’ kwa kutiliana saini, kama vitabainika havina tatizo lolote vitumike kwa kupandikiza watu wengine.

“Tanzania bado hatuna sheria hiyo na tunatarajia kupeleka mapendekezo hayo serikalini Bunge liyatungie sheria,” alisema Dk. Nyangasa.

Alisema mwaka 2016 ulifanyika uchunguzi wa tiba kwa wagonjwa 973 na kati yao, 620 walipatiwa matibabu ya moyo  bila kufungua kifua kupitia mishipa ya damu kwa kutumia mtambo wa ‘Catheterization’ na upasuaji wa kufungua kifua ulifanyika kwa wagonjwa 353.

MAREKANI

Nchini Marekani, kila baada ya dakika 10 mtu mmoja huwekwa kwenye foleni ya watu wanaosubiri kuwekewa moyo mpya kuweza kuendelea kuishi. 

Hali hiyo hutokea baada ya moyo wa mgonjwa kuonekana hauwezi kufanyiwa matibabu na hivyo njia pekee ya kuokoa maisha yake ni kupata moyo mpya ambao huwekewa kwa njia ya upasuaji (transplant).

Shirika la Umoja wa Kuchangia Viungo Marekani, linasema takriban watu 22 hufariki dunia kila siku nchini humo wakiwa katika foleni ya kusubiri mtu wa kujitolea moyo kuokoa maisha yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles