23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Infinix yajivunia simu mpya ya Infinix Note 30

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu ya Infinix imeeleza kuwa mauzo ya simu mpya ya Infinix NOTE 30 Series yamevunja rekodi ikiwa ni wiki chahe tu tangu kuzinduliwa kwake jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo mapema leo Juni 12, jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa toleo hilo ambalo lilienda sambamba na promosheni kubwa ya #Gusanishaijae limevunja kabisa rekodi ya mauzo ambayo iliwekwa na kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Infinix, Promosheni ya GusanishaIjae imebeba maana halisi ya teknolojia ya Fast Chaji iliyopo kwenye simu hizi, Infinix NOTE 30 Pro imefanyiwa uwekezaji mkubwa wa teknolojia ya Fast chaji ikiwa na WATT68 Pamoja na Wireless Fast Chaji ya WATT15.

“Ubunifu haujaishia hapo Infinix NOTE 30 Pro ina Reverse Charge kuchajisha kifaa chochote chenye kutumia Wireless lakini pia unaweza endelea na matumizi huku ukiwa unaichaji pasipo kupata moto.

Infinix NOTE 30 Pro ziliuzika kwa wingi sana hapo jana katika soko kuu la simu ‘Kariakoo’ kwa nchini Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa kutoka @infinixmobiletz zawadi kubwa ambayo ilitoka siku ya promosheni hiyo ni kitita cha Sh 1,000,000,” imeeleza taarifa hiyo.

Kulingana na Infinix, sifa nyingine za simu hii ni Megapixel 108 Triple camera, AMOLED Display, 120Hz na Chipset MediaTek Dimensity 8050, unaweza kuipata kwa Sh 650,000 kwa kulipia papo hapo au kwa mkopo kwa kiasi ichoicho pasipo Riba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles