Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Kampuni ya simu Infinix imeshirikiana na kampuni ya Mawasiliano Vodacom Tanzania kuzindua simu mpya ya Infinix ZERO ULTRA 5G.
Simu hiyo ilizinduliwa Alhamisi Oktoba 14, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo mtandao wa Vodacom utatoa ofa ya GB96 za internet na dakika 2,400 za maongezi na fursa ya kununua simu hiyo kupitia malipo kidogo kidogo kwa muda wa miezi 3 hadi 12.
Kwa mujibu wa washirika hao, simu hiyo ya Infinix ZERO ULTRA 5G ni ya kwanza duniani kuja na wati 180 yenye kujaza chaji kwa dakika 12 tu, simu hii imeanza kupatikana sokoni kwa bei ya Sh 1,300,000 tu,” amesema
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Samwel kutoka Vodacom amesema simu hiyo mpya aina ya Infinix Zero Ultra 5Gina uwezo mkubwa unaokwenda sambamba na mtandao wao wa kasi ya 5G.
“Kama mnavyofahamu kwamba Vodacom tunafanya vizuri katika nyanja ya mawaisiliano ya simu za mkononi hapa nchini na ndiyo sababhu pia tukashirikiana na wenzetu wa Infinix ambao wameuwa wakitengeneza simu nzuri zinazoenda na teknolojia ya kisasa na zenye kuruhusu kasi ya juu ya internet hususan 5G.
“Hivyo, mteja wa Vodacom Tanzania akinunua simu hii aina ya Infinix Zero Ultra 5G katika maduka yetu makubwa nchini na katika maduka ya Infinix, sisi Vodacom tunampa mteja huyu GB 8 na dakika 200 kwa mwezi, na hivyo kufanya mteja atakayenunua simu hii kupata jumla ya GB 96 na dakika 2,400 kwa mwaka mzima,’’ amesema Samwel.
Upande wake mwakilishi kutoka Infinix, Jessica James amesema kuwa: “Tunafuraha kushirikiana na Vodacom Tanzania kuzindua simu pendwa ambayo inaiwakilisha kampuni hii ya Infinix kwa sasa ‘Infinix ZERO ULTRA 5G.
“Simu hii pendwa ndio simu nambari moja yenye kuchukua muda mfupi kujaa chaji na tunaamini kupitia ushirika huu na Vodacom wateja wetu watafurahia simu hii katika swala la speed ya internet pia bila ya kuwasahau wapenzi wa mapicha picha na video Infinix ZERO ULTRA 5G inauwezo wakuchukua picha kwa wakati moja kupitia kamera ya mbele na ya nyuma yenye megapixel 200 na teknolojia ya OIS’,” amesema Jessica.
Upande wake Mkufunzi katika maswala ya teknolojia, Given Edward amesema: “Infinix imeingia sokoni kwa kishindo kikubwa kupitia ZERO ULTRA 5G simu yenye sifa hizi; chaji wat 180, kamera ya megapixel 200, kioo cha FHD+ AMOLED 3D muundo wa kujipinda na refresh rate 120Hz ambavyo ni bora kwa kurekodi video, kunasa picha na kuchukua muda mfupi kwa simu kujaa chaji.
“Licha ya kuwa na teknolojia ya kisasa kwa kila feature nimefurahishwa na gharama ya simu hii, Infinix imerahisishia kizazi cha leo ambacho kipendelea kujiendeleza kupitia teknolojia kufanya hivyo. Kampuni imefaulu kwa asilimia 100 kuleta mabadiliko makubwa katika soko la simu kupitia simu hii,” amesema Edward.