24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

INDONESIA: WANAKIJIJI WAUA MAMBA 300 KULIPIZA KISASI

Wanakijiji wenye hasira kali wawauwa mamba 300 kwenye makao ya wamyama katika mkoa wa West Papua nchini Indonesia.

Muuaji hayo yalikuwa ni kwa ajili ya kulipiza kisasi kifo cha mwanamume mmoja ambaye aliuawa na mamba mmoja eneo hilo.

Maafisa na polisi wamesema kuwa hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka.

Kwa mujibu wa Mamlaka husika, kuuliwa kwa wanyama wanaolindwa ni hatia na inaweza kusababisha kifungo nchini Indonesia.

Mwanakijiji huyo aliuawa siku ya Ijumaa asubuhi alipokuwa akitafuta mboga eneo la kuzalia mamba.

Mmoja wa wankijiji aliyekuwa karibu na eneo la tukio, alisikia mtu akiomba msaada na alipofika huko aliona mamba akimshambulia mtu.

Baada ya mazishi siku ya Jumapili, mamia kadhaa ya wanakijii wenye hasira walielekea eneo la makao ya wanyama wakiwa wamejihami kwa visu, chuma, nyundo na sururu.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles