30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

India kufanya uchaguzi mwezi ujao

NEW DELHI, India

TUME ya Uchaguzi nchini hapa, imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu  utafanyika mwezi ujao ambao utakuwa ni wa kidemokrasia katika taifa hili na huku ikionekana kwamba, Waziri Mkuu, Narendra Modi, ataibuka mshindi kutokana na mgogoro uliopo baina ya nchi hii na Pakistan.

Akizungumza jana mjini hapa, Msemaji wa tume hiyo, Sunil Arora, alisema uchaguzi utafanyika Aprili 11, mwaka huu na utawahusisha wapigakura milioni 900 na kwamba  kati yao, milioni 15 ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 19.

Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, tatizo la uhaba wa ajira na kushuka kwa bei ya bidhaa za kilimo, vilishusha umaarufu wa Waziri Mkuu Modi, lakini wapigakura wanasema Chama Tawala cha  Bharatiya Janata Party (BJP), kitawapiku wapinzani wake baada ya mwezi uliopita jeshi la hapa kuingia vitani na wapinzani wa nchi hii, Pakistan na kinaweza kujizolea mamilioni ya kura kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

“Kwa mara ya kwanza nitampigia kura  Narendra Modi kwa sababu nimefurahishwa na anachokifanya dhidi ya  Pakistan,” alisema Anjali Tivari wakati akimchukua mwanawe kutoka shuleni katika Mji wa Mumbai.

“Nimefurahi sana amewapa jibu sahihi  Pakistan,” aliongeza mpigakura huyo.

Akizungumzia uchaguzi huo, Waziri Mkuu Modi alielezea mafanikio ya Serikali  na akaelezea kufurahishwa kwake na mwitikio wa watu kujiandikisha kupiga kura.

“Nina matumaini utashuhudiwa uchaguzi wa kihistoria kwa watu wengi kujitokeza. Ninaweza kuuita ni wa kihistoria kwa  idadi kubwa ya watu kujitokeza,” aliandika  Modi kupitia ukurasa wake wa Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles