24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Imran Khan: Hatutaki magaidi waweke makazi Pakistan

ISLAMABAD, PAKISTAN

WAZIRI Mkuu wa Pakistan Imran Khan amesema kuwa haitoruhusu genge lolote la kigaidi kuendesha shughuli zake nchini humo na kusisitiza kuwa nchi hiyo sio makazi ya magaidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA limesema kuwa Imran Khan amesema hayo mbele ya wafuasi wake kusini mwa Pakistan na kuongeza kuwa, serikali yake haitowaruhusu magaidi kutumia ardhi ya nchi hiyo kushambulia nchi jirani.

Matamshi hayo ya Waziri Mkuu wa Pakistan yamekuja siku chache tangu ulipopamba moto mzozo baina ya nchi hiyo na India kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyowalenga wanajeshi wa India.

Mzozo mpya katika uhusiano wa Pakistan na India ulizuka baada ya kundi la kigaidi linalojiita Jaish al Muhammad kushambulia wanajeshi wa India huko Kashmir tarehe 14 mwezi ulioisha wa Februari na kuua wanajeshi 44.

Jeshi la India lilituma ndege zake na kushambulia baadhi ya maeneo ndani ya ardhi ya Pakistan likidai kuwa ni maficho ya magaidi hao. Pakistan nayo ilijibu mashambulizi hayo ya India kwa kutungua ndege mbili za nchi hiyo na kumteka nyara rubani mmoja wa India ingawa baadaye ilimuachilia huru ili kuonesha nia yake njema.

Siku moja kabla ya kushambuliwa wanajeshi wa India basi lililokuwa limebeba walinzi wa mpakani wa Iran lilishambuliwa huko Zahedan, makao makuu ya mkoa wa Sistan na Baluchistan wa Iran unaopakana na Pakistan na kusababisha maafisa 27 wa Iran kuuawa na wengine 13 kujeruhiwa.

Kundi la kigaidi la Jaish al Dhulm linaloendesha shughuli zake katika ardhi ya Pakistan lilijigamba kuhusika na shambulio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles