30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

IMF yataka benki kuboresha huduma

Thomas Baunsgaard
Mwakilishi Mkazi wa IMF, Thomas Baunsgaard

NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Fedha la Kimataifa (IMF) limeitaka sekta ya benki nchini kuboresha huduma ili kuhakikisha inaendelea kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mwaka 2013 kuhusu Sekta ya Benki Afrika Mashariki iliyotolewa na Kampuni ya Ernst & Young, Mwakilishi Mkazi wa IMF, Thomas Baunsgaard, alisema sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kuchangia Pato la Taifa (GDP).

Alisema kutokana na umuhimu wa sekta hiyo kuna haja ya kuendelea kuboreshwa ili kuhakikisha inapata wateja wapya.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ernst & Young, Chacha Winami, alisema bado kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo zikiwamo gharama kubwa za kufanya biashara na kupata leseni.

“Kuna changamoto nyingi zinazokwamisha ukuaji wa sekta ya benki kama kupata hatimiliki na suala la utakatishaji fedha haramu,” alisema Winami.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Ernst & Young, Joseph Sheffu, alisema anaamini yapo masuala mengine ambayo Serikali ikiongeza juhudi na kuyatilia mkazo baadhi ya changamoto zitapungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles