30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ilemela kufikisha elimu ya afya ya uzazi shuleni

Na Yohana Paul, Mwanza

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Plan international na Kiwohede imejipanga kufikisha elimu ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupitia elimu ya stadi za maisha ili kuwaepusha na mimba za utotoni.

Akizungumuzia mpango huo Afisa Ustawi wa Jamii Hamashauri ya jiji la Mwanza, Davis Justine amesema hadi sasa tayari wameshaanza kuongea na wanafunzi kuwaelezea umuhimu wa wao kujilinda na kuwaelewesha njia thabiti za wao kujizua kutopata ujauzito wakiwa mashuleni

Justine alisema ili kufanikisha adhima ya mradi huo tayari wamefungua klabu za wanafunzi mashuleni ambao watakuwa mabalozi wa elimu ya uzazi lengo ni kuandaa kizazi ambacho ni salama sambamba na kuongeza hamasa kwa wazazi ama walezi kuwa na uwezo wa kuwalinda watoto wao.

“Kama ofisi ya ustawi wa jamii kazi yetu kubwa ni kuhakikisha jamii inakuwa katika misingi bora na amani, kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa kwa ujumla, tumeshiriki sana kuelimisha jamii kuanzia tukiwa ofisini.

“Tuna kesi nyingi sana za matunzo ya watoto, unakuta mzazi mmoja ana watoto wanne au zaidi ya watano, ukiangalia suala zima la malezi, wao kama wazazi wengi wanapata changamoto kwa sababu ya  kuzaa bila mpangilio,” alisema.

Justine alisema ili kuondokana na changamoto hiyo wanaendelea kuhimiza kila mtu kuzaa watoto ambao atakuwa anaweza kuwalea na kuwahudumia sambamba na kuwaelimisha wanandoa waweze kujua ni namna gani wataweza kutumia njia za uzazi wa mpango kuweza kupunguza malamiko ya malezi na ongezeko la watoto wa mitaani.

Akizungumuzia suala la watoto wa mitaani Justine alisema halmashauri hiyo inaendelea kushirikiana na  Mashirika ya Railyway children, Wotesawa na Kiwohede ili kufanya juhudi za kuwaunganisha na familia zao, kuwaelimisha namna bora ya kujikinga na aina yeyote ya ukatili na kuwapatia bima ya afya iliyoboreshwa (CHF).

Afisa Maendeleo Manispaa ya Ilemela, Sarah Ntangu alisema ili kuwezesha mapinduzi kwenye masuala ya afya ya uzazi, wanaendelea kujikita zaidi kutoa elimu ya kujitambua, kwa vjana na mabinti ambao wapo kwenye makundi rika na barehe kwani ndio waathirika aidi wa changamoto za afya ya uzazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles