28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ilemela kinara umiliki makazi holela nchini

Benjamin Masese -ilemela

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza, imeendelea kuongoza katika urasimishaji na makazi holela nchini kwa kuandaa michoro ya mipango miji 58,000, kupima viwanja 52,000 na kumilikisha viwanja 72,000.

 Hayo yameelezwa juzi na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula  wakati akisimamia ugawaji hati miliki za viwanja 1,508 kwa wananchi wa Wilaya ya Ilemela.

 Dk. Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, alisema  ameridhishwa na kasi ya upimaji na umilikishwaji ardhi unaofanywa na wataalamu wa Wilaya ya Ilemela  huku  akiwaasa wananchi waliokabidhiwa hati zao kumshukuru na kumpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuridhia kufanyika zoezi hilo.

 “Binafsi nafurahi kuona pamoja na changamoto zote mlizonazo, bado Wilaya ya Ilemela inaongoza katika zoezi la urasimishaji nchini, wilaya hii ndiyo imekuwa ikitolewa mfano na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

“Wapo wanaodhani na kusema mcheza kwao hutunzwa wakiwa na maana mimi kama Naibu Waziri wa Ardhi napendelea kwangu, la hasha isipokuwa ni malengo na uwajibikaji wa pamoja kati ya wananchi na watumishi Idara ya Ardhi, nawataka wananchi wa wilaya zingine waliorasimishiwa  makazi yao wahakikishe wanalipia,” alisema Dk. Mabula.

 Hata hivyo, Dk. Mabula alizikumbusha kampuni za upimaji zinazoendesha zoezi la urasimishaji makazi kutekeleza agizo la  Lukuvi la kukamilisha kazi zote zilizobaki ili kwenda  sambamba na kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuwaondolea adha wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles