Na Denis Sinkonde, Songwe
Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amepiga marufuku wanunuzi wa zao la parachuchi na pareto wasiokuwa na vibali wilayani humo kuja na kununua pareto kwa wakulima bila kufuata utaratibu wa Serikali.
Amesema serikali ya wilaya itafanya msako kwa wanunuzi ambao wanawakandamiza wananchi kwa kununua bei isiyo halali.
Marufuku hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya kupokea kero ya wakulima wa mazao hayo katika vijiji vya Ibaba na Itale ambapo walisema kuwa wamekuwa wakiuza kwa walanguzi wasiokuwa na vibali jambo ambalo linawanyonya wakulima ambao hutegemea mazao hayo kiuchumi.
Gidarya amesema baadhi ya walanguzi kutoka kampuni iitwayo TAN-EXTRA ambayo ilianza kununua pareto kwa njia za ‘panya’ hununua zao hilo ndani ya wilaya hiyo bila kuwa na kibali sambamba na bei inayowakandamiza wakulima hao, nakwamba hivyo watu wajanja wanaodhurumu wananchi kununua bei ya udalali wa mazao hayo kwa wakulima watakamatwa.
Gidarya amesema kazi ya serikali ni kumlinda mkulima kunufaika, lakini zimejitokeza kampuni ambazo zinawaingilia wananchi kupitia Wilaya Mbeya vijijini mkoa wa Mbeya kuwapa mbegu ambazo hazifai kwa wakulima na baadaye kununua kwa bei ambayo imawaumiza.
“Tutahakikisha tunawakamata walanguzi wote kupitia makampuni yote ambayo yananunua kwa bei ambayo siyo elekezi hivyo niwatake wananchi muuze kwenye vikundi kwa bei ambayo itatangazwa hapo baadaye.
“Watendaji wa vijiji na kata hakikisheni wanunuzi wa zao la parachichi wanaripoti kwenye ofisi za vijiji na kusaini mikataba itakayomnufaisha mwananchi na tani ambazo makampuni hayo yatanunua kwa msimu,” amesema Gidarya na kuongeza kuwa:
“Nakuagiza Afisa Kilimo Wilaya hakikisha unaanza msako wa kukamata kampuni zilizonunua parachi kwa wakulima kwa bei ya hasara na kukwepa kulipa ushuru ili walipe fidia na ikiwezekana kampuni zilizopo zisaini mkataba,” amesema Gidarya.
Upande wake Afisa Kilimo wilayani hapa, Godlike Mndeme amesema baada ya kubaini kuwapo kwa kampuni ya TAN-EXTRA kuwalangua wakulima walilotoza faini na mpaka sasa wapo kwenye mchakato wa kuanda mkataba wa ununuzi wa zao hilo huku akionyakampuni nyingine zinzofanya hivyo.
Godlike alisema kwa upande wa ununuzi wa zao la parachichi wilaya ya Ileje kuna kampuni mbili zinzotambulika za BAYOFRESHI na KUZA-AFRIKA hivyo wananchi waripoti ofisi za kijiji pindi kampuni nyingine zinapoingia kiholela kununua mazao yao.
Wakizungmza kwaniaba ya wananchi wa kata hizio baadhi ya wakulima wameiomba serikali kuongeza na kuruhusu wanunuzi wengine ili waweze kuuza kwa urahisi na bei iongezeke.
Baadhi ya kata zinazolima zao la Pareto ni Itale, Ibaba, na baadhi ya vijiji vya kata ya Bupigu na Kalembo. Uzalishaji wa zao hilo wilayani Ileje kwa Mwaka 2020/2021 ni tani 590.