23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ilala wamchangia Samia fomu ya urais

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji amewaongoza wananchi wa kata hiyo kuchanga Sh milioni moja kumwezesha Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji, akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Amana, Dar es Salaam.

Khimji ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi CCM Taifa amewasilisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi uliofanyika katika Kata ya Ilala na kukabidhi cheti cha pongezi kutambua mchango uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kata hiyo na maeneo mengine nchini.

Akizungumza Agosti 21,2024 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Amana, amesema miradi mbalimbali imetekelezwa katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara na mingine.

“Tunatambua msimamo wa chama chetu kwamba mgombea pekee atakayepeperusha bendera ya urais mwakani ni mheshimiwa mama Samia Suluhu Hassan, wana Ilala tunamuahidi hatutamuangusha.

“Ilala tunampenda mama Samia, tuko watu 12,500 tutajitokeza kumpigia kura na tutapita sehemu mbalimbali kumsemea mama kutokana na mambo mazuri aliyoyafanya katika nchi yetu,” amesema Khimji.

Naibu Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu, amesema Rais Samia amefanya juhudi kubwa kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi CCM inatekelezwa kwa vitendo hivyo anastahili kuungwa mkono katika uchaguzi mkuu ujao.

“Rais Samia ndiye anayesimamia na kutoa fedha zote za miradi inayoendelea nchini, anatuongoza kwa upendo kuhakikisha Watanzania tunazidi kusonga mbele…tunajipanga kuhakikisha tunashinda chaguzi zote, tuko ‘serious’ na tutamfikia kila mtu,” amesema Zungu.

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Amana, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally Said amesema; “Hatuhitaji tochi kuona barabara, shule au zahanati zilizojengwa. Tusipoteze kura hata moja kwa mama Samia na viongozi wengine wa CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles