26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

IGP Wambura amuelewa Rais Samia kuhusiana na haki

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura ametaja mikakati yake ambayo amesema atahakikisha inatekelezwa ikiwamo kuhakikisha uhalifu unakoma, maadili ndani ya Jeshi hilo na haki kwa wananchi.

IGP Wambura amebainisha hayo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuapishwa Jumatano Julai 20, 2022 katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Miongoni mwa mikakati aliyoieleza ni pamoja na kukomesha uhalifu na kuzingatia haki na maadili.

Ikumbukwe kuwa IGP Wambura ameapishwa kuchukua nafasi ya Simoni Sirro ambaye ameteuliwa na kuapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Mara baada ya kuripoti Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma akitokea Ikulu ya Chamwino alipoapishiwa, IGP Sirro amesema mikakati hiyo mikubwa atahakikisha inatekelezwa kwa kushirikiana na makamishna walio chini yake na kada mbalimbali za askari pamoja na viongozi waliopo katika Jeshi la Polisi.

“Kwanza ni kuhakikisha suala la uhalifu, mapambano dhidi ya uhalifu yanaimarishwa na suala la uhalifu, wahalifu wasije wakafiriki kwamba ile ni ajira hakuna hiyo na nguvu ambayo tutatumia kupambana na uhalifu ni akili kubwa, nguvu kubwa lakini nguvu ya kisasa,” amesema IGP Wambura

“Na tutahakikisha wananchi wanakuwa salama na Serikali inaweza kuendelea na shughuli zake na kutokuwa na fikra za kuona ni namna gani wataanza tena kushughulika na uhalifu na kuweka rasilimali zao pale,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles