30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

IGP SIRRO AWAONYA WALIOPATA MSAMAHA WA RAIS SIKUKUU YA MUUNGANO

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amewaonya watu waliopata msamaha wa Rais Dk. John Magufuli, katika sikukuu wa Muungano Aprili 26, mwaka huu kuchunga tabia na matendo yao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 24, wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa vituo vya polisi vya kisasa vya Mburahati, Kiluvya, Gogoni na Mbweni IGP Sirro amesema nia ya rais kuwapa msamaha ilikuwa njema lakini kuna baadhi ya watu wameitumia vibaya fursa hiyo na hadi sasa watu watano wamekwishauawa na wananchi.

“Rais aliwapa msamaha baadhi ya watu lakini wametumia vibaya msamaha huo na kurejea kwenye matendo yao maovu ambapo  hadi sasa watu watano wamekwishauawa na wananchi kutokana na matendo yao.

“Ukitoka gerezani kwa msamaha, maana yake umerekebisha mwenendo wako na wananchi wanatarajia uwe hivyo, lakini kama ukifanya vinginevyo, Serikali isilaumiwe,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles