32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Ifahamu aina hii ya ugonjwa wa kifafa

NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM


KICHWA  kuangukia kifuani (nodding syndrome) kwa muda mrefu imechukuliwa kwenye jamii kwamba hutokea kutokana na mtu kukumbwa na pepo au kupandisha mashetani.

Hata hivyo, watafiti wamethibitisha kwa kutumia vifaa vya kisasa kwamba dhana hiyo ni potofu, hiyo ni aina mpya ya ugonjwa wa kifafa iliyogundulika kwa mara ya kwanza 1960, katika Kijiji cha Mahenge, mkoani Morogoro.

Aina hiyo ya kifafa pia iliwahi kutokea miaka ya 1980 Liberia, Cameroon, Sudani Kusini na Magharibi mwa Uganda miaka ya 2000 hata hivyo uthibitisho kwamba ni ugonjwa haukuwepo wakati wote huo.

Imeelezwa aina hiyo ya kifafa huonekana zaidi kwenye sehemu ambapo kuna wadudu wa Onchocerciasis lakini uhusiano wake bado unafanyiwa utafiti wa kina.

Hayo yalielezwa jana na Profesa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Idara ya Magonjwa ya Ndani, William Matuja wakati alipokuwa akiwasilisha chapisho lake hilo, chuoni hapo.

“Duniani watu wanaoishi na kifafa ni zaidi ya milioni 60, idadi huongezeka watu 34 hadi 76 kwa 100,000 kila mwaka, Afrika asilimia kubwa ya watu wanaoishi na kifafa ni 20 hadi 58 kwa kila watu 1000.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifafa barani Afrika na dunia kwa ujumla, katika vijiji vya mahenge idadi ni kubwa kufikia watu 37.5 kwa kila watu 1000, hivyo kuna zaidi ya watu milioni moja nchini ambao wanaugua kifafa,” alisema.

Aidha alisema ukioainisha umri wa wagonjwa wa kifafa nchini wapo katika hatari ya kifo mara sita zaidi kulinganisha na jamii yote kwa ujumla.

Alisema zaidi ya asilimia 60 ya vifo vinasababishwa na athari za ugonjwa wa kifafa moja kwa moja au kwa namna nyingine.

Alisema wagonjwa wa kifafa cha aina hiyo ni vijana wakiwa na umri wa wastani wa miaka 15.4, zaidi ya asilimia 24 ya wagonjwa wa kifafa wana ulemavu mwingine na wengi hutokana na kuangukia moto wakati mgonjwa anapopata degedege.

“Idadi kubwa ya watu wana imani potofu kuhusu kifafa na zaidi ya asilimia 36 bado wanaamini kwamba ugonjwa huu unatokana na nguvu za giza,” alisema.

Alisema miongoni mwa jamii pia bado inaaminika ni ugonjwa wa kuambukiza na asilimia 50 ya wagonjwa wa kifafa hupata msongo wa mawazo na kukosa furaha.

 

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,400FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles