22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

‘IEBC KUBADILI TAREHE YA UCHAGUZI WA MARUDIO’

NAIROBI, KENYA

UAMUZI iwapo tarehe ya uchaguzi wa urais wa marudio ibadilishwe ulitarajiwa kufanywa jana na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ingawa uamuzi huo hautarajiwi kutangazwa hadi kesho Jumatano.

IEBC ilikutana baadaye jana kujadili pamoja na mambo mengine ripoti kuhusu usajili wa wapiga kura na mfumo wa kielektroniki wa usambazaji matokeo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, IEBC ilitarajia kuonana na Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu  Raila Odinga katika Kituo cha Taifa cha kujumuisha kura cha Bomas of Kenya.

Kampuni ya Ufaransa ya OT-Morpho iliwasilisha kwa mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ripoti ya kurasa sita ikieleza muda utakaotumika kupanga upya vifaa 45,000 kwa uchaguzi mpya, ambao umepangwa kufanyika Oktoba 17.

“Kwa vile  Morpho imeshafafanua kilichomo katika ripoti hiyo kwa mdomo, mjadala wa kubadili tarehe umeonekana kutoepukika, ingawa bado haujawa ajenda kamili,” chanzo kimoja cha kuaminika cha habari ndani ya IEBC kimesema.

Chanzo hicho kimesema tume imepanga baadaye jana kuijadili kikamilifu ripoti hiyo ya Morpho na kutoa uamuzi wa masuala kadhaa pengine ikiwamo tarehe ya uchaguzi.”

Miongoni mwa mabadiliko ya lazima ni kuweka majina mawili tu ya wagombea wawili wa urais badala ya wanane waliokuwapo awali.

Lengo ni kuepuka kasoro na hatari za mfumo kutumia takwimu kutoka uchaguzi uliofutwa.

Kwa vile pia utahusisha wagombea wawili tu wa ngazi ya urais, majina ya wagombea 14,000 wa viti vingine vitano, itabidi matokeo yao na picha ziondolewe kutoka mfumo huo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles