26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Idrisa Sultan afutiwa kesi

Na Brighiter Masaki,Mtanzania Digital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Mchekeshaji Idrisa Sultan(27) na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kurusha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Sultani ameachiwa huru na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Rubologa baada ya wakili wa Serikali Neema Mushi kudai kuwa DPP amewasilisha Nolle chini ya kifungu cha 91(1) cha CPA kuonesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Hakimu Rubologa amesema kwa kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo, mahakama yake inakubali ombi la Jamhuri inawaachia huru washtakiwa.

 Mbali na Idrisa, washtakiwa wengine ni Doctor Ulimwengu(28) na Isihaka Mwinyimvua(22).

Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya Machi 8,  2016 na Machi 12, 2020 sehemu tofauti tofauti  jijini  Dar es Salaam washitakiwa hao, walirusha maudhui online tv  kwenye akaunti ijulikanayo Loko Motion bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini( TCRA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles