Idris: Samatta ameniongezea safari za Ulaya

0
684

Jessca Nangawe

KITENDO cha staa wa soka Tanzania, Mbwana Samatta kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England, kimepokelewa kwa shangwe na staa mwenzake Idris Sultan huku akidai kimemwongezea safari za Ulaya.

Samatta ameacha gumzo kwa Watanzania wengi baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo.

Idris ambaye ni mshindi wa Big Brother Afrika mwaka 2014, alisema ni jambo la furaha kwa Watanzania wote na yeye akiwa mmoja wa mashabiki zake atakua akimfuatilia kwa karibu ikiwemo kusafiri na kwenda kumshuhudia mubashara akicheza.

“Ni jambo la kujivunia kwa Watanzania wote, kitendo hicho kimezidi kuipaisha Tanzania kimataifa, sasa tunajulikana duniani, nadhani kwa mimi ameniongezea safari za Ulaya, nitakwenda kumtazama Live,” alisema Idris.

Aidha Idris amesisitiza Serikali ya Tanzania inapaswa kumtumia staa huyo kama sehemu ya kujitangaza zaidi ikiwemo kumpa sapoti ya kutosha kwani kwa sasa amekua balozi mzuri wa soka la Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here