Idris amuomba radhi rais Magufuli

0
1017

BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM. 

MSANII wa Vichekesho nchini, Idris Sultan ameomba radhi kwa kitendo cha kutumia picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufiri, kwenye mitandao yake ya kijamii.

Msanii huyo aliitumia vibaya picha ya rais akidai lengo lake kubwa lilikuwa kumtakia heri siku yake ya kuzaliwa, mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Sultani alisema, hakufanya kwa nia mbaya bali alifanya kwa mapenzi mema ya kumtakia heri rais katika kumbukizi ya kuzaliwa kwake.

“Mimi ni mchekeshaji, lakini nitumia nafasi hii kumuomba radhi rais wangu, viongozi pamoja na watanzania wote kwa nilicho kifanya, sikufanya kwa nia mbaya bali nilifanya kwa mapenzi mema ya kumtakia heri,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here