Na Mwandishi Wetu
Idara ya Uhamiaji nchini imethibitisha kuwapa uraia wa Tanzania kwa Tajnisi wachezaji watatu wa kigeni wa timu ya Singida Black Stars.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara hiyo leo, wachezaji waliopewa Emmanuel Kwame Keyekeh(Ghana), Josephat Arthur Bada(Ivory Coast) na Muhamed Damaro( Guinea).
