26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

IDADI YA WANAFUNZI KIMATAIFA YAPUNGUA MAREKANI

Na JOSEPH LINO


HALI ya kisiasa nchini Marekani, hasa katika zuio la wageni kuingia nchini humo, inaweza kuathari sekta ya elimu katika vyuo vikuu.

Tatizo hilo limegusa upande wa wanafunzi kutoka mataifa mengine ambao wanajiunga vyuo vikuu vya Marekani.
Wakati muda cha kutuma maombi ya kujiunga vyuo vikuu vya Marekani unaendelea, idadi ya wanafunzi wa kimataifa imepungua.

Mwaka huu baadhi vyuo vya elimu ya juu wamegundua kuwapo kwa upungufu wa wanafunzi wa kimataifa wanaotuma maombi.

Kumekuwapo upungufu mkubwa kwa maombi ya kujiunga chuo kwa wanafunzi kutoka China, India na nchi za Mashariki ya Kati kwa asilimia 40 katika vyuo vingi nchini Marekani.

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na taasisi ya American Association of Collegiate Registrars, unaonyesha wasomi, waajiri na maofisa wa shule wanasema mtazamo wa wanafunzi wa kimataifa umebadilika dhidi ya Marekani.

Maofisa wanasema utawala wa serikali na idara ya uhamiaji kuhusiana na kuzuia wageni kutoka kwa baadhi ya nchi kuingia Marekani umeleta athari kubwa.

Vyuo vikuu vya nchini Marekani huwa vinategemea wanafunzi wa kimataifa katika kuongeza sifa ya chuo.
Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wa kimataifa mwaka 2016 ilifikia takribani milioni moja, ambayo ilizalisha ajira 400,000, kwa mujibu wa Association of International Educators.

Pia kupungua kwa kujiandikisha kwa wanafunzi wa kimataifa katika vyuo vikuu kutaathiri uchumi wa Marekani, ambapo wanafunzi wa kimataifa huchangia mapato ya dola za Mareakani bilioni 32.

Mwaka jana peke yake, wanafunzi kutoka China walichangia mapato ya kiasi cha dola bilioni 11 katika uchumi wa Marekani, wakati India ilichangia kiasi cha dola bilioni 5.

Wanafunzi wa kimataifa nchini Marekani hulipa ada kamili ambayo inasaidia kupunguza gharama ya ada kwa wanafunzi kutoka taifa hilo.

Baadhi ya wataalamu wa elimu ya juu wameonya kuwa, kupungua kwa wanafunzi wa kimataifa kutasababisha kuondoa baadhi ya kozi, ada ya juu na kupoteza baadhi ya taaluma.

“Nilifikiri kwa hatua hii, ni vigumu kuwafikia na kushawishi wanafunzi na wazazi kwamba elimu ya Marekani bado ni bora,” ripoti inasema.

Mwanafunzi kutoka China, Zhou Linli, ambaye anasoma Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA), anasema kibaya zaidi ni sintofahamu ya kupata chaguo la chuo bora kutokana na hali ilivyo sasa.

“Natumaini chuo changu kitanisaidia kutatua matatizo yanayotokana na sera za utawala wa serikali ya sasa,” alisema.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani na Benki ya Dunia, unaonyesha kwamba, Marekani inapoteza sehemu ya wahamiaji wasomi ambao wanakwenda Uingereza, Canada, Australia, Norway na Mexico kwa kipindi cha takribani mwongo mmoja.

Kuhamia kwa vipaji vya kimataifa nchi nyingine ni habari njema kwa vyuo vikuu ambavyo vipo nje ya Marekani na habari mbaya kwa sekta ya ubunifu wa nchi hiyo.

Wachambuzi wa uchumi wanasema kuna uhusiano mkubwa kati ya wahamiaji na kuinuka kwa sekta ya teknolojia ya nchini Marekani.

Kufikia Februari mwaka jana, zaidi ya nusu ya makampuni yenye mtaji wa dola bilioni moja yalianzishwa na wahamiaji nchini humo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles