30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Idadi ya waliofariki shambulio la Virginia yafikia 13

Virginia, Marekani

Idadi ya watu waliofariki kwenye shambulio la bunduki katika Mji wa Virginia nchini Marekani imefikia 13 akiwamo mshambuliaji aliyeuawa katika mashambulizi na polisi.

Mshambuliaji huyo anayedaiwa kuwa ni mfanyakazi wa Idara ya Nishati na Maji ya Mji wa Virginia, aliwafyatulia risasi wafanyakazi wenzake jana Ijumaa na kuwaua watu 12 na kuwajeruhi wengine wanne kabla ya kuuliwa na polisi.

Mkuu wa polisi ya Virginia, James Cervera amesema mshambuliaji alitumia bunduki iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti pamoja na kasha kadhaa za risasi alizotumia wakati wa shambulizi hilo.

Shambulio hilo katika fukwe za mapumziko mjini Virginia linatajwa kuwa baya kabisa miongoni mwa matukio ya uhalifu wa kutumia bunduki nchini Marekani tangu shambulizi la mwezi Novemba mwaka jana ambapo watu kadhaa waliuawa mjini Los Angeles.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles