25.6 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Idadi ya wagonjwa wa kisukari duniani yaongezeka

Veronica Romwald, Dar es Salaam



Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, amesema takwimu  za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kasi ya idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kisukari duniani inaongezeka.

Amesema hayo wakati akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatano Novemba 14, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kisukari.

“Asilimia 80 ya wagonjwa wanatoka nchi zilizo na kipato cha chini, mwaka 2017 inaeleza watu milioni 425 waliugua na idadi hiyo huenda itaongezeka kufikia watu 592 mwaka 2035 ikiwa hatua hazitachukuliwa,” amesema.

Aidha, amesema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pekee inahudumia wagonjwa wapatao 6,000 kwa mwaka wenye kisukari.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Museru amewatoa hofu Watanzania wanapopewa rufaa kwenda kutibiwa katika hospitali hiyo, Tawi la Mloganzila na kuongeza kuwa hospitali hiyo ina vifaa vya kutosha zaidi ya Muhimbili.

“Kuna vifaa vingi zaidi ya kule Upanga, madaktari bingwa nao tunao, kulikuwa na wasiwasi awali wagonjwa walipopewa rufaa kuja kutibiwa Mloganzila, waje wasiwe na wasiwasi watapata matibabu ya uhakika,” amesema.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homoni wa Muhimbili, Banduka Elisante, ametaja mambo yanayochangia kuongezeka kwa ugonjwa huo ambao upo katika kundi la magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni mabadiliko ya taratibu za mtindo wa maisha kwa ujumla.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles