Idadi ya wagonjwa wa corona nchini yaongezeka

0
1236
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema imethibitika uwepo wa wagonjwa wawili wa virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo katika Maabara kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii.

Amesema mgonjwa wa kwanza ni mwanamume (61) raia wa Marekani anayeishi jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa amewekwa chini ya uangalizi maalumu kwa ajli ya taratibu za kitaalamu na mwingine pia ni mwanamume (24) raia wa Ujerumani aliyepo visiwani Zanzibar.

Kuhusu mgonjwa wa Zanzibar, Waziri Ummy amesema taarifa zaidi zitatolewa na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid.

Hadi sasa idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini imefikia watatu ambapo mgonjwa wa kwanza aliyegundundulika kuwa na maambukizi mkoani Arusha ni mwanamke.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here