24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Iceland yamwachisha kazi Roy Hodgson

Roy Hodgson
Roy Hodgson

NICE, UFARANSA

KOCHA wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson, ametangaza kuachana na timu hiyo baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Iceland kwenye michuano ya Euro 2016.

Hodgson mwenye umri wa miaka 68, ameweka wazi kwamba hawezi kuendelea kuwa na timu hiyo baada ya kutolewa katika hatua ya 16 bora nchini Ufaransa.

Katika mchezo huo, England ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa nahodha wake, Wayne Rooney, kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya nne, kabla ya Ragnar Sigurdsson kusawazisha katika dakika ya sita, wakati huo, Kolbeinn Sigthorsson akiongeza bao la pili katika dakika ya 18.

“Huu ni muda wangu wa kumpisha kocha mwingine ambaye atawaza kuendeleza maendeleo ya timu hii yenye wachezaji wengi ambao wana uwezo mkubwa, ninaamini kila ukiwapa majukumu lazima watekeleze.

“Wachezaji wapo kwa ajili ya taifa lao, lakini matokeo yakiwa tofauti ni kutokana na makosa ya kimchezo, lakini ninaamini hakuna timu ambayo inataka kupoteza michezo yake.

“Jambo la mwisho ni kwamba napenda kuwashukuru wale wote ambao walikuwa nami katika kipindi chote wakiwa chama cha soka pamoja na mashabiki kwa kipindi chote cha miaka minne nilikuwa hapa.

“Samahani kwa kuamua kujiuzulu mara baada ya kutolewa katika michuano mikubwa kama hii, lakini hili ni jambo ambalo linatokea, lakini jambo ambalo ninaweza kulisema ni kwamba nawatakia kila la heri katika maendeleo ya soka na ninaamini muda mfupi ujao tutaiona England ikiwa katika fainali ya michuano mikubwa,” alisema Hodgson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles