30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ibueni changamoto zinazoendelea mitaani-Florah

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Jamii imetakiwa kuibua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kucha tabia ya kufumbia vitendo viovu.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Machi 18, na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Florah Luhala, wakati wa kufunga warsha ya siku tano iliyoandaliwa na Matandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushirikiana na Vituo vya Taarifa na Maarifa.

Mgeni rasmi pamoja na washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Meya, Florah amewataka wawakilishi wa Kata za Manispaa hiyo kuhakikisha kuwa wanakuwa wa kwanza katika kutoa taarifa na kuibua changamoto zote zikiwamo zile zinazowakabili watoto.

Amesema iwapo watatoa taarifa itakuwa ni rahisi kwa wahusika wa vitendo hivyo kuweza kuchukuliwa hatua.

“Tumekuwa na warsha nzuri ambayo imeibua mijadala mbalimbali na kutujengea ufahamu, ombi langu kwenu niwatake mnapokwenda kwenye majumbani mkawe mstari wa mbele katika kuibua changamoto mbalimbali.

“Kwani kumekuwa na matukio mengi kwenye jamii lakini sisi wenyewe tumekuwa tukiyafumbia mamcho, hivyo mkatumie maarifa haya mliyoyapata kuibua changamoto hizo ili tuweze kuwa kitu kimoja.

“Kwani bila kushirikiana baina ya pande zote itakuwa ni ngumu kuweza kufikia lengo ya kutokomeza ukatili katika jamii, hivyo makatumie elimu hii kuleta matokea chanya,” amesema Florah.

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo, akiwamo Luthi Kiwika kutoka Kata ya Kivule akizungumza na www.mtanzania.co.tz amesema maarifa waliyoyapata hapo yamewafungua macho ikiwamo namna nzuri ya kuibua changamoto katika jamii.

“Ni wazi kuwa warsha hii imeweza kunifumbua macho kwa mambo ambayo nilikuwa siyajui, hivyo nitaitumia vizuri katika kuhakikisha jamii inakuwa salama.

“Mfano katika eneo la bajeti za kata tumejifunza kwamba tunatakiwa kutoa mawazo yetu jambo ambalo awali hatukulifahamu, pia imetujengea uwezo wa kuthubutu,” amesema Luth.

Upande wake Zuwena Urembo kutoka Kata ya Kivule, amesema kwa siku hizo tano amepata elimu namna ya kukabili changamoto.

Naye Joseph Safari kutoka Kata ya Majohe, amesema kuwa kuwa amejifunza juu ya mchango alio nao katika kuchangia maendeleo ya kata na jamii yake ikiwamo kupitisha bajeti.

Warsha hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiku ya Wanawake Duniani iliyoadhimisha Machi 8, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles